You are here: Home NEWS Local News

Local News

News

HANS VAN DER PLYUM KUINOA YANGA

VIEWED 4024 TIMES

Hans Van Der Plyum ameingia mkataba wa kuinoa Young Africans kuanzia leo na moja kwa moja kesho mchana ataungana na wachezaji wake waliopo nchini Uturuki kwenye kambi ya mafunzo ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa baadae.

Last Updated on Monday, 13 January 2014 22:15

Read more...

 

News

YANGA KUIVAA ALTAY SK

VIEWED 2302 TIMES

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara na vinara wa ligi hiyo timu ya Young Africans itashuka dimbani siku ya jumatano kucheza mchezo wa pili wa kirafiki wa kujipima nguvu na timu ya Altay S.K iliyopo Ligi Daraja la Pli nchini Uturuki.

Last Updated on Monday, 13 January 2014 18:37

Read more...

 

News

MKWASA AENDELEZA DOZI

VIEWED 2980 TIMES

Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 jana dhidi ya timu ya Ankara Sekerspor, kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa ameendelea kuwanoa vijana wake katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach Side iliyopo pembeni kidogo ya mji wa Antalya katika eneo la mji wa Manavgat.

Last Updated on Sunday, 12 January 2014 18:56

Read more...

   

News

YANGA YAICHAPA 3 - 0 ANKARA SEKERSPOR

Young Africans imeanz vizuri katika kambi yake ya mafunzo nchini Uturuki baada ya kuifunga timu ya Ankara Sekerspor kwa mabao 3-0, mchezo uliofanyika pembeni kidogo ya eneo ililofikia katika mji wa Manavgat Antalya.

Kocha wa Young Africans aliwatumia wachezaji 18 jumla katika mchezo huo ambao wenyeji mara baada ya mchezo walimpongeza kwa timu yake kwa kucheza vizuri katika mchezo huo wa kirafiki.

Dakika ya 10 ya mchezo shuti lililopigwa na mganda Emmanuel Okwi lilishinda mlinda mlango wa Ankara Sekerspor ambapo aliutema mpira huo na kumkuta Didier Kavumbagu aliyeukwamisha mpira huo wavuni na kuhesabu bao la kwanza.

Timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Ankara Sekerspor i0 - 1 Young Africans .

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na iliwachukua dakika moja Young Africans kujipatia bao la pili la mchezo kupitia kwa Emmanuel Okwi aliyeitumia vyema pasi ya mwisho ya kiungo Mrisho Ngasa aliywatoka walinzi wa Ankara Sekaspor na kumpasia mfungaji ambaye hakufanya makosa na kuukwamisha mpira wavuni.

Dakika ya 58 kocha Mkwasa alifanya mabadiliko, ambapo waliingia Hamis Kizza na Nizar Khalfani kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na kiungo Hassan Dilunga.

Hamis Kizza aliipatia Young Africans bao tatu la mchezo na la ushindi dakika ya 61 ya mchezo baada mpira aliogongewa na Domayo kuwapita walinzi wa Ankara Sekerspor na kumkuta Kizza ambaye alipiga shuti liliomgonga mlinzi wa Ankara Sekerspor wakati akiokoa na kujaa wavuni.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Ankara Sekerspor 0 -3 Young Africans.

Mara baada ya mchezo kaimu kocha mkuu wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa alisema anashukuru vijana wake walicheza vizuri kwa kufuata malekezo na ndio maana wakaweza kupata ushindi huo,makosa yapo machache yaliyojitokeza na ataendelea kuyafanyia kazi.

"Mechi ilikua ni nzuri ukizingatia ndo mchezo wetu wa kwanza wa kirafiki tukiwa na siku ya tatu tangu tufike hapa Uturuki, kwa mazoezi ya jana vijana wameosha mabadiliko na leo wameweza kucheza vizuri na kuweza kupata ushindi, kikubwa naamini kwa siku zilizobakia nitaendelea kufanya marekebisho na kukifanya kikosi kuendelea kuwa bora pindi kitaporejea nchini tayari kwa mzunguko wa pili wa Lig Kuu ya Vodacom" alisema Mkwasa

Kikosi cha Young Africans kilichocheza leo ni:

1.Juma Kaseja/Ally Mustafa "Barthez" (dkk 65), 2.Juma Abdul, 3.Oscar Joshua/David Luhende(dkk 82), 4.Mbuyu Twite (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Frank Domayo/Ibrahim Job(dkk 80), 7.Haruna Niyonzima/Saimon Msuva (dkk72), 8.Hassan Dilunga/Nizar Khalfan (dkk 58), 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kizza (dkk 58), 10.Mrisho Ngasa/Jerson Tegete (dkk 68), 11. Emmanuel Okwi/Said Bahanuzi (dkk 85)

 

News

YANGA YAICHAPA 3-0 ANKARA SEKERSPOR

VIEWED 5243 TIMES

Young Africans imeanza vizuri katika kambi yake ya mafunzo nchini Uturuki baada ya kuifunga timu ya Ankara Sekerspor kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika pembeni kidogo ya eneo ililofikia katika mji wa Manavgat Antalya.

Last Updated on Saturday, 11 January 2014 18:31

Read more...

   

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1342
mod_vvisit_counterYesterday11260
mod_vvisit_counterThis week20331
mod_vvisit_counterLast week35641
mod_vvisit_counterThis month75921
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1464644

We have: 93 guests, 2 bots online
Your IP: 207.241.237.102
Mozilla 5.0, 
Today: Feb 14, 2014