You are here: Home NEWS Local News 22 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA CHAD

22 WAITWA TAIFA STARS KUIVAA CHAD

E-mail Print PDF
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo ametangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu jijini N’Djamena. Mchezaji aliyeitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Mwandini Ally wa Azam huku pia akimjumuisha kwenye kikosi chake mshambuliaji wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Thomas Ulimwengu. Kikosi kamili ni makipa Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya), Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Godfrey Taita (Yanga) na Juma Jabu (Simba). Viungo ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Ramadhan Chombo (Azam) na Shomari Kapombe (Simba). Washambuliaji katika kikosi hicho ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada), Mrisho Ngassa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden), Hussein Javu (Mtibwa Sugar) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC). Timu itaingia kambini Novemba 3 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na inatarajiwa kuondoka nchini Novemba 9 mwaka huu kwenda N’Djamena kwa ajili ya mechi hiyo. Stars na Chad zitarudiana Novemba 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Last Updated ( Saturday, 05 November 2011 12:19 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday11100
mod_vvisit_counterYesterday4839
mod_vvisit_counterThis week23420
mod_vvisit_counterLast week36083
mod_vvisit_counterThis month74419
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1463142

We have: 95 guests, 8 bots online
Your IP: 207.241.237.223
Mozilla 5.0, 
Today: Feb 13, 2014