Mchezaji wa kimtaifa kutoka nchini Zambia Davies Mwape leo ameibuka shujaa baada ya kupeleka kilio Msimbazi, kwa kufunga bao moja na la ushind kwa timu yake ya Young Africans.
Mwape alifunga bao hilo dakika ya 74 ya mchezo kufuatia makosa yaliyofanywa na mabeki wa simba Juma Nyoso na Victor Costa.
Simba iliweza kucheza vizuri kipindi cha kwanza lakini kipindi cha pili Young Africans iliutawala zaidi mchezo na hasa baada ya mabadiliko yaliyofanywa na kocha Kostadian Papi kuwatoa Hamis Kiiza na Davies Mwape na nafasi zao kuchukuliwa na Idrisa Rashid na Jeryson Tegete.
Viungo wa kati Haruna Niyonzima akishirikina na Juma Seif Kijiko na Nurdin Bakari waliutawala sana mchezo na kuwafunika Partick Mafisango, Jerry Santo na Mwinyi Kazimoto.
Upande wa ulinzi Nadir Haroub Canavaro alionyesha kiwango cha hali ya juu kwa kuweza kuwadhibiti washambuliaji wa Simba akisaidiwa na Godfrey Taita, Chacha Marwa na Oscar Joshua.
Kenneth Asamoah aliongoza safu ya ushambuliaji akisaidiwa na Hamis Kiiza na Davies Mwape ambao kwa pamoja walionekana kuisumbua ngome ya Simba..
Mpaka mwamuzi anamaliza mpira Young Africans wameibuka na ushindi wa bao moja kwa bila na kufikisha pointi 24 nyuma ya Simba inayoongoza ligi kwa pointi 27.
Kocha mkuu Kostadin Papic amekisifu kikosi chake kw akucheza kwa kuelewana na kupata ushindi katika mchezo wa leo.















