VIEWED 3973 TIMES
Wawakilishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya Young Africans leo imeanza vizuri mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni kutoka visiwa vya Comoro katika mchezo uliofanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ikicheza mbele ya mashabki wake takribani elfu 17 katika Uwanja wa Taifa, kikosi cha Young Africans kiliweza kucheza vizuri na kutumia nafasi hizo ambapo imeweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata kutokana na kuhitaji droo tu ya aina yoyote.
Mrisho Ngasa aliwainua mashabiki wa Young Africans vitini dakika ya 13 ya mchezo kufuatia kuukwamisha mpira wavuni kwa kichwa baada ya pasi ya iliyopigwa na mlinzi wa kulia Mbuyu Twite kumkuta mfungaji na kuumwamisha mpira wavuni bila makosa.
Dakika ya 20 ya mchezo, nahodha wa Young Africans Nadir Haroub "Cannavaro" aliipatia Young Africans bao la pili kwa kichwa baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende kuunganisha moja kwa moja wavuni.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 2 - 0 Komorozine de Domoni.
Kipindi cha pili kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo Didier Kavumbagu aliiingia kuchukua nafasi ya David Luhende.
Dakika ya 58 Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao la tatu baada ya kumalizia pasi safi ya Mrisho Ngasa aliyewatoka walinzi wa Komorozine de Domoni upande wa kulia na kumpasia Kavumbagu ambaye aliukwamisha mpira wavuni.
Hamis Kiiza "Diego" aliwainua mashabiki wa Young Africans vitini dakika ya 59 ya mchezo kufuatia pasi ya Didier Kavumbagu aliywatoka walinzi wa Komorozine de Domoni.
Mrisho Ngasa aliipatia Young Africans bao la tano dakika ya 65 ikiwa ni dakika moja baadae baada ya kazi nzuri iliyofanywa na na viungo wa Young Africans Haruna Niyonzima na Frank Domayo.
Dakika tatu baadae Mrisho Ngasa aliifungia Young Africans bao la sita na likiwa ni bao bao lake la tatu katika mchezo wa leo baada ya kumalizia mpira wa Saimon Msuva uliokoloewa na golikipa wa Komorozine.
Dakika ya 81 ya mchezo, Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao saba kufuatia kuitumia vizuri pasi ya mshambuliaji Hamis Kiiza ambapo Kavumbagu bila ajizi alimchambua mlinda mlango wa timu ya Komorozine.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 7- 0 Komorozine de Domoni.
Mchezo wa marudiano utafanyika wiki ijayo kati ya tarehe 14,15,16 Februari Visiwa vya Comoro ambapo Young Africans inahitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kusonga mbele kutofungwa mabao zaidi ya 6-0 katika mchezo huo.
Kocha wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema anshukuru vijana wake wamecheza vizuri, wamepata nafasi za kufunga wamezitumia japo sio zote, kikubwa tutaendelea na mazoezi kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa leo.
Young Africans: 1.Juma Kaseja 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Kelvin Yondani/Rajab Zahir, 6.Frank Domayo "Chumvi", 7.Saimon Msuva/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima, 9.Hamis Kiiza, 10.Mrisho Ngasa, 11.David Luhende/Didier Kavumbagu




















