VIEWED 2565 TIMES

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans imewasili salama katika jiji la Tanga majira ya saa 6 kasorobo ikitokea jijini Dar es salaam tayari kwa kuwakabili wenyeji timu ya Coastal Union siku ya jumatano katika Uwanja wa Mkwakwani.
Msafara wa watu 30 ukiwa na wachezaji 20, umewasili jijini Tanga na kufikia katika hotel ya Central City ambayo ndio huwa wanafikia siku zote na kikosi cha kocha mholanzi Hans Van Der Pluijm jioni kimefanya mazoezi katika viwanja vya Gymkana eneo la Raskazone kujiandaa na mchezo huo.
Kocha Mkuu Hans sambamba na wasaidizi wake Charles Mkwasa na Juma Pondamali wamesema wamekuja na kikosi kilichokamilika na kushirikiana kwa pamoja na benchi la ufundi wanaamini kitaibuka na ushindi hiyo siku ya jumatano.
Kikosi kilichopo jijini Tanga ni
Makipa: Juma Kaseja, Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende, Mbuyu Twite, Kelvin Yondani, Rajab Zahir na Nadir Haroub "Cannavaro"
Viungo: Haruna Niyonzima, Hamis Thabit, Nizar Khalfan na Haruna Niyonzima
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Hussein Javu na Said Bahanuzi




















