You are here: Home NEWS Local News YANGA YAWASILI DAR, KUIVAA ASHANTI KESHO

YANGA YAWASILI DAR, KUIVAA ASHANTI KESHO

E-mail Print PDF

VIEWED 2942 TIMES

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania bara Young Africans tayari wameshawasili salama jijini Dar es salaam wakitokea jijini Antalya nchini Uturuki walipokuwa wameweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya klabu Bingwa Afrika barani Afrika.

Young Africans imetua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyeree majira ya saa 9:30 alfajiri kwa shirika la ndege la Turkish Airline na moja kwa moja kikosi cha wachezaji 27 na benchi la Ufundi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo wa kesho.

Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Plyum amesema anashukuru kikosi chake kimefika salama jijini Dar es salaam na amesema vijana wake watafanya mazoezi mepesi leo jioni kabla ya kesho kushuka dimba la Uwanja wa Taifa.

Akiongelea kambi ya Antalya Hans amesema kambi ilikuwa nzuri na mafanikio makubwa kwani vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika nidhamu, kujituma, upendo na kushirikiana kitu ambacho ndio nguzo ya timu kufanya vizuri.

Aidha Hans amewaomba wanachama wa Young Africans, wapenzi na washabiki kesho kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu yao iliyokuwa kambini Uturuki itakapocheza na wauza mitumba wa Ilala Ashanti United na kuitambulisha staili yao ya uchezaji kutoka Antalya.

 

Last Updated ( Friday, 24 January 2014 06:24 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday3321
mod_vvisit_counterYesterday7098
mod_vvisit_counterThis week34603
mod_vvisit_counterLast week44755
mod_vvisit_counterThis month49519
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1438242

We have: 58 guests, 4 bots online
Your IP: 207.241.237.224
Mozilla 5.0, 
Today: Feb 09, 2014