You are here: Home NEWS Local News YANGA KUMALIZA NA OLJORO

YANGA KUMALIZA NA OLJORO

E-mail Print PDF

VIEWED 741 TIMES

Young Africans itakamilisha ratiba ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara kwa kucheza na timu ya maafande wa jeshi la kujenga Taifa nchini JKT Oljoro siku ya alhamis katika dimba la Uwanja wa Taifa jijjini Dar es salaam.

Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Bora -Kijitonyama kujiandaa na mchezo huo wa keshokutwa ambao ni muhimu kwa watoto wa jangwani kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi.

Kocha Ernie Brandts amesema vijana wake wanaendelea kuimarika na kuyashika vizuri mafunzo yake, kwa jinsi timu ilivyo kwa sasa anaamini vijana wake hakuna timu ya kuizua Yanga kutetea Ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo.

"Ni kweli nina majeruhi kadhaa amabao wameshindwa kufanya mazoezi kutokana na majeraha mbalimbali, wengine afya zao zimeendelea kuimarika na wanaweza kurejea dimbani wakati wowote kuanzia kesho" alisema Brandts .

Kikubwa nachoshukuru Yanga safari hii ina kikosi kilichokamilika, nina zadi ya wachezaji watatu katika kila nafasi hivyo pamoja na kuwa na majeruhi zaidi ya wachezaji wanne bado huwezi kuona pengo lolote kutokana na vijana wote kuwa fit'

Wachezaji ambao bado wanaendelea na matibabu ni David Luhende, Nizar Khalfani na Salum Telela ambao wamekuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili sasa, huku Juma Abdul, Bakari Masoud wakisubira ruhusa ya daktari juu ya kuanza kwao mazoezi.

Ikiwa imecheza michezo 12 ikishinda michezo saba, sare michezo minne na kupoteza mchezo mmoja, Young Africans imejikusanyia pointi 25 katika nafasi ya tatu zikiwa ni pointi moja nyuma ya vinara wanaongoza Ligi timu za Azam FC na Mbeya City kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Safu ya ushambuliaji ya Young Africans imefanikiwa kutikisa nyavu za wapinzani mara 28 huku ikiwa imefanikiwa kupata bao katika kila mchezo ilioucheza na kuonyesha kuwa washambuliaji wake ni moto wa kuotea mbali.

Hamis Kiiza ana mabao nane (8) huku Mrisho Ngassa & Didier Kavumbagu wakiwa na mabao matano (5) kila mmoja, Jerson Tegete mabao manne (4) wakati Saimon Msuva, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nizar Khalfani na Frank Domayo wakifunga bao moja moja.

Upande wa ulinzi umeruhusu mabao 11 na tangu mwalimu afanyie marekebisho safu imeimarika kwani mpaka sasa imecheza jumla ya michezo mitatu (3) pasipo kuruhusu nyavu zake kutikiswa na wapinzani.

Last Updated ( Tuesday, 05 November 2013 11:18 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday2529
mod_vvisit_counterYesterday4523
mod_vvisit_counterThis week18295
mod_vvisit_counterLast week27012
mod_vvisit_counterThis month62091
mod_vvisit_counterLast month96545
mod_vvisit_counterAll days1027418

We have: 34 guests, 8 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Nov 16, 2013