You are here: Home NEWS Local News MEYA ILALA AKUTANA NA VIONGOZI WA YANGA

MEYA ILALA AKUTANA NA VIONGOZI WA YANGA

E-mail Print PDF

VIEWED 1752 TIMES

Meya wa Manisapaa ya Ilala jijini Dar es salaam mstahiki Jerry Silaa leo amepokea maombi ya klabu ya Young Africans kuhusu kuomba eneo la ziada kwa ajili ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa uwanja wa kisasa eneo la Jangwani.

Mara baada ya kupokea barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe, Silaa alisema yeye pamoja na wenzake hawaoni sababu ya kuzuia harakati hizo za maendeleo na faida kwa wananchi wa mkoa wa Dar es salaam.

"Kwanza viongozi wa Yanga poleni sana kwa kuchelewa kufika, nilikuwa nawasubira wenzangu naibu meya pamoja na mwenyekiti wa mipango na makazi wa manispaa ili tuje kuonana na nyie pamoja, kwa kifupi suala lenu litafanyiwa kazi na kufikia mwezi ujao Novemba tayari tutakua tumeshawapatia majibu" alisema Silaa.

Wazee wangu, wanachama pamoja na viongozi suala hili nalikabidhi kwa mwenyekiti wa mipango ili aliwasilishe kwenye kikao cha madiwani na kufikia mwezi ujao tayari majibu yatakua yameshapatikana ili muweze kuendelea na mchakato huo wa maendeleo kwa watanzania.

Akisoma maelezo ya barua mwenyekiti wa bodi ya wadhamini alisema, tumeshangoea na watu wa mazingira na wamesema wapo tayari kusaidiana na sisi ila kikubwa ni tulikua tunasubiri majibu kutoka manispaa ya Ilala juu ya eneo la ziada tulioliomba.

Mara baada ya kikao hicho cha pamoja katibu wa baraza la wazee mzee Ibrahim Akilimali alitoa shukrani kwa mstahiki meya pamoja wasaidizi wake kwa kuweza kukutana na viongozi wa Yanga na kutoa ahadi ya kulimaliza suala lao la eneo la ziada haraka iwezekavyo

 

Last Updated ( Friday, 18 October 2013 20:43 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday2560
mod_vvisit_counterYesterday2890
mod_vvisit_counterThis week10041
mod_vvisit_counterLast week36083
mod_vvisit_counterThis month61040
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1449763

We have: 75 guests, 2 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Feb 12, 2014