Kocha mkuu Papic amewaambia wapenzi na wanachama wa timu ya Yanga kuwa kikosi cha timu hiyo kipo tayari kukabiliana na mnyama Simba katika pambano la mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
pambano linalotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kesho majira ya saa 10. Jioni.Papic amesema pamoja na kwamba ameichukua timu hiyo katika kipindi kifupi timu yake ni bora kutokana na wachezaji waliosajiliwa msimu huu.
Kocha huyo amesema kikosi cha Yanga alichokiacha mwaka jana na hivi sasa kinatofauti kutokana na wachezaji wengi waliopo sasa wana vipaji na uwezo wa kusakata kandanda.
Kocha huyo amesema mfumo atakaoutumia katika pambano hilo ndio utakaoimaliza timu ya Simba kwa kuwa ana imani nayo Simba imejiandaa vya kutosha katika pambano hilo.
“Msiwe na wasiwasi kikosi changu kizuri kina vijana wanojituma kina uwezo mkubwa wa kuisambaratisha Simba” alisema Papic.
Pambano hilo lenye kugusa hisia mbalimbali kwa wapenzi na mashabiki wa soka hapa nchini linatarajiwa kuwa kali na la kusisimua kutokana na timu hizo kufanya maandalizi ya kutosha kwa kipindi kirefu.




















