You are here: Home NEWS Local News YANGA, PRISONS ZATOKA SARE

YANGA, PRISONS ZATOKA SARE

E-mail Print PDF

VIEWED 801 TIMES

Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya wenyeji timu ya Prisons FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa jioni ya leo katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Kikosi cha Young Africans kiliingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 mbele ya maafande wa magereza Prisons FC lakini hazikuzaa matunda kwani timu ya wanyapara ilisimama imara kuhakikisha haipotezi pointi nyumbani.
Dakika za mwanzo Saimon Msuva na Didier Kavunmbagu walikosa mabao ya wazi na kuokuwa kwao makini kulifanya timu ziende mpaka dakika 30 za kipindi cha kwanza zikiwa sare ya kutofungana.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 41 ya mchezo akimalizia pasi safi ya winga wa kulia Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Prisons na kuminina krosi hiyo iliyomkuta mfungaji na kuukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza, Prisons 0 - 1 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kuanza kwa kasi kw alengo la kusaka bao la mapema, washambuliaji wa Young Africans bado waliendelea kukosa umakini katika umaliziajia.
Dakika ya 77 Peter Michael aliipatia Prisons bao la kusawazisha kwa kichwa baada ya mpira wa kona uliopigwa na kiungo Omega Seme kumkuta mfungaji na kuukwamisha mpira wavuni moja kwa moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Prisons 1 - 1 Young Africans.
Kocha wa Yanga Ernie Brandts amesema wachezaji wake kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri na kusababisha makosa mengi lakini kutokua makini pia kwa washambuliaji wa Prisons kulifanya timu yetu kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa bao 1.
Young Africans itondoka kesho alfajiri tayari kwa safari ya kurejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wake unaofuata dhidi ya timu ya Azam FC siku ya jumamosi.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar Khalfani, 8.Salum Telela/Frank Domayo, 9.Jerson Tegete/Said Bahanuzi, 10.Didier Kaavumbagu, 11.Haruna Niyonzima
Last Updated ( Wednesday, 18 September 2013 19:17 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday3373
mod_vvisit_counterYesterday3691
mod_vvisit_counterThis week15643
mod_vvisit_counterLast week18037
mod_vvisit_counterThis month72278
mod_vvisit_counterLast month77292
mod_vvisit_counterAll days860382

We have: 40 guests, 2 bots online
Your IP: 207.241.237.211
Mozilla 5.0, 
Today: Sep 28, 2013