You are here: Home NEWS Local News YANGA YAJIANDAA KUIVAA MBEYA CITY

YANGA YAJIANDAA KUIVAA MBEYA CITY

E-mail Print PDF

VIEWED 966 TIMES

Kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola - Mabibo jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wake wa tatu wa Ligi Kuu dhidi ya timu iliyopanda daraja ya Mbeya City septemba 14 jijini Mbeya.

Young Africans ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa na poin 4 baada ya kucheza michezo miwili ikishinda mmoja, sare mmoja na kufunga jumla ya mabao 6 na kufungwa mabao mawili ikiwa ni pointi mbili nyuma ya vinara wanaongoza ligi JKT Ruvu Staars.

Baada ya kutoka sare ya bao 1 -1 dhidi ya timu ya Coastal Union katika mchezo uliofanyika katikati ya wiki kwenye dimba la uwanja wa Taifa, Young Africans itamkosa huduma ya mshambuliaji wake wa pembeni Saimon Msuva kwenye mchezo huo kufuatia kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi Martin Saanya.

Kocha Mkuu Ernie Brandts ameendelea kuyafanyika kazi makosa yaliyojitokeza katika mchezo dhidi ya Coastal Union lengo ni kuhakikisha kikosi kinakua safi kuelekea kwneye mchezo huo dhdi ya Mbeya City mwezi ujao.

Wachezaji wote wapo safi kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mbeya City na wameendelea na mazoezi kujiaanda na michezo mwili mfululizomkoani Mbeya dhidi ya timu za Mbeya City na Prisons FC.

 

Last Updated ( Friday, 30 August 2013 11:16 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1893
mod_vvisit_counterYesterday4570
mod_vvisit_counterThis week8054
mod_vvisit_counterLast week15238
mod_vvisit_counterThis month9835
mod_vvisit_counterLast month77292
mod_vvisit_counterAll days797939

We have: 6 guests, 4 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Sep 04, 2013