You are here: Home NEWS Local News KUELEKEA NGAO YA JAMII, YANGA YAENDELEA KUJIFUA

KUELEKEA NGAO YA JAMII, YANGA YAENDELEA KUJIFUA

E-mail Print PDF

VIEWED 1734 TIMES

Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Young Africans kimeendelea na mazoezi katika viwanja vya shule ya sekondari Loyola kujiaanda na mchezo wa Ngao ya Hisani siku ya jumamosi Agosti 17, 2013 dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans wanakutana na Azam FC katika mchezo ambao Yanga wanahitaji kuendeleza wimbi la ushindi kufuatia kuwa imeshinda michezo yake mitatu mfululizo dhidi ya wana lamba lamba Azam FC kwa msimu uliopita.

Kocha mkuu Brandts ameendelea kuwanoa vijana wake kuhakikisha wanaedelea kuwa fit kiakili, kimwili na kiafya na morali waliyonayo waendelea kuwa katika kiwango cha juu na kupata ushindi katika michezo inayokuja.

Wachezaji wote wamefanya mazoezi leo na habari njema ni kurejea kwa mshambuliaji wake Hamis Kiiza aliyekuwa nchini Uganda kwa kambi ya timu ya Taifa kabla ya jana kuja kunganana wenzake kuiandaa na mchezo huo.

Katika michezo mitatu iliyopita Yanga dhidi ya Azam FC, watoto wa Jangwani wameshinda michezo yote mitatu, mchezo wa kwanza fainali ya Kagame 2-0, mzunguko wa kwanza 2-0 na mzunguko wa pili 1-0 sawa na

P3 W3 D0 L0 GF5 GD 0 PTS9.

Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni:

walinda mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida; na Issa Kazembe

Walinzi wa pembeni: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua na David Luhende

Walinzi wa kati : Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani 'Cotton', Rajab Zahir, Ibrahim Job

Viungo: Salum Telela, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfani, Hamis Thabit, Bakari Masoud

Washambuliaji wa Pembeni: Mrisho Ngassa, Saimon Msuva, Abdallah Mguhi 'Messi'

Washambuliaji wa kati: Said Bahanuzi, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Shaban Kondo, Hussein Javu na Jerson Tegete

 

NB: Haruna Niyonzima jana amejiunga na timu ya Taifa ya Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopo kwenye kalenda ya Fifa dhidi ya Malawi na anatarajiwa kurejea siku ya alhamis mara baada ya mchezo huo wa siku ya jumatano kuungana na wachezaji wenzake.

Last Updated ( Tuesday, 13 August 2013 12:33 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday473
mod_vvisit_counterYesterday4636
mod_vvisit_counterThis week473
mod_vvisit_counterLast week48441
mod_vvisit_counterThis month104504
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1493227

We have: 33 guests, 2 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Feb 18, 2014