You are here: Home NEWS Local News NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA

NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA

E-mail Print PDF

VIEWED 6345 TIMES

Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Mwalusako leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.

Naye mwenyekiti wa mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema anashukuru kwa Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.

Kwa kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.

Aidha Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na kunishangilia pia.

Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu yangu ya Yanga.

Ngsa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia Yanga katika msimu ujao.

DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)

EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)

 

Last Updated ( Monday, 20 May 2013 18:48 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1609
mod_vvisit_counterYesterday1465
mod_vvisit_counterThis week5627
mod_vvisit_counterLast week18037
mod_vvisit_counterThis month62262
mod_vvisit_counterLast month77292
mod_vvisit_counterAll days850366

We have: 30 guests, 6 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Sep 25, 2013