You are here: Home NEWS Local News UPEMBUZI YAKINIFU KAUNDA STADIUM WAKAMILIKA

UPEMBUZI YAKINIFU KAUNDA STADIUM WAKAMILIKA

E-mail Print PDF

VIEWED 5747 TIMES

Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani.

Kaimu meneja wa kampuni ya BCEG Zhang Chengwei David amesema upembuzi yakinifu umekamilika kuhusiana na suala la ujenzi wa uwanja mpya wa klabu ya Yanga eneo la jangwani ambapo taratibu za makadirio na michoro imekamilika tayari na leo kuwasilishwa kwa uongozi wa klabu ya Yanga.

Zhang alisema kwamba kampuni yao BCEG wana uzoefu wa ujenzi wa viwanja sehemu mbali mbali duniani, na mfano mzuri ni ujenzi wa uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam ambao ulikua mkubwa kuliko viwanja vyote barani Afrika kabla ya kujengwa kwa uwanja mpya wa nchini Afrika Kusini (Soccer city) uliotumika kwa ajili ya fainali za kombe la dunia 201o.

Aidha Zhang aliendelea kusema pia kwa sasa wanajenga uwanja wa Uhuru Stadium (jirani na uwanja wa Taifa ) ambapo ujenzi wake ulianza mwaka jana mwezi Aprili na wanatarajia kuukamilisha mapema mwaka huu, huku ukiboreshwa kwa kufunikwa uwanja mzima na kuweka viti ambayo vitaweza kubeba watazamaji 20,000.

Katika uwasilishaji huo wa makadirio ya ujenzi wa uwanja wa Kaunda, mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa klabu ya Yanga Francis Kifukwe alisema wanafurahishwa na kampuni ya BCEG kwa kukamilisha zoezi la upembuzi yakinfu mapema ambapo leo wamepata fursa ya kujionea na kujua maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.

Kufukwe alisema wamepewa nafasi ya kuchangua aina tatu za uwanja, uongozi wa klabu ya Yanga utakaa na kuchagua aina mojawapo ambayo wataiwasilisha kwa kampuni ya BCEG na mwishoni mwa mwezi Mei wanatarajia kusaini mktaba kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda.

Akijibu swali la waandishi wa habari juu ya jinsi gani wataweza kupata fedha za ujenzi wa uwanja, Kifukwe alisema ujenzi wa uwanja mpya utajengwa na wanachama, wapenzi na washambiki wa klabu ya Yanga.

Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.

Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo.

 

 

Last Updated ( Friday, 05 April 2013 08:30 )  
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Kikosi cha Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Gombani kujiandaa na mchezo wake wa mwisho... http://t.co/xF73xqFibQ
yanga1935: Somewhere in Pemba Island http://t.co/Q8sX0Dgxx7
yanga1935: Young Africans Players in Camp at Pemba Island @Yanga1935 http://t.co/LfnUq2WFth
yanga1935: Kikosi cha mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 timu ya Young Africans Sports Club leo... http://t.co/c7khKLYUF2
yanga1935: Kuelekea mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young Africans limeomba mwamuzi wa mchezo... http://t.co/cPwQS4GOrs
yanga1935: Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans leo imeendelea na mazoezi katika... http://t.co/7aSEeYlWu1
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday559
mod_vvisit_counterYesterday1956
mod_vvisit_counterThis week4450
mod_vvisit_counterLast week15395
mod_vvisit_counterThis month29101
mod_vvisit_counterLast month60138
mod_vvisit_counterAll days518131

We have: 11 guests, 4 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: May 16, 2013