You are here: Home NEWS Local News YANGA, POLISI ZATOKA SARE

YANGA, POLISI ZATOKA SARE

E-mail Print PDF

VIEWED 943 TIMES

Young Africans ambayo inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu wa 2012/2013 leo imetoka sare ya 0-0 dihi ya timu ya Polisi Morogoro katika mchezo uliofanyika leo jioni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Katika mchezo huo uliohudhuriwa na washabiki wengi wa soka kutoka mkoa wa Dar es salaam na mikoa ya jirani, umeishia kwa sare hiyo ya pasipo kufungana huku mwamuzi wa mchezo huo Dominic Nyamisana na wasaidizi wake wakishindwa kulimudu pambano hilo kutokana na kutokua makini.

Watoto wa jangwani waliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kupata bao la mapema na katika dakika ya tatu mchezo, Hamis Kiiza alishindwa kuipatia Yanga bao la kuongoza kutokana na kutokua makini katika umaliziaji.

Polisi nayo ilijaribu kufanya mashambulizi ya kushtukiza lakini umakini wa walinzi wa Yanga ulikuwa kikwazo kwao kuweza kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'

Yanga iliendelea kufanya mashambulizi langoni mwa timu ya Polisi lakini kutokua makini kwa washambuliaji wa Yanga Saimon Msuva, Said Bahanuzi, Hamis Kiiza na Nizar Khalfani ulishindwa kuipatia Yanga bao .

Mpaka mpira unakwenda mapumziko, wenyeji Polisi Morogoro 0 - 0 Young Africans.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko kwa kumuingiza Stephano Mwasika aliyechukua nafasi ya Nizar Khalfani, mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa timu ya Yanga ambapo iliweza kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Polisi.

Baada ya Yanga kuwa inafanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Polisi na kusababisha kupata kona nyingi mfululizo, wachezaji wa Polisi waliamua kuwa wanajiangusha kila dakika ili kupoza kasi ya mchezo huku mwamuzi akionekana kutokujali kwa tabia hiyo ya wachezaji.

Polisi waliendelea kucheza kwa kupoteza muda hali iliyopelekea kupoteza radha ya mchezo, dakika za majeruhi Yanga ilifanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa Polisi lakini mashambulizi hayo hayakuweza kuipatia bao.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Polisi Morogoro 0 - 0 Young Africans.

Kwa matokeo hayo ya leo Young Africans inaendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom baada ya kufikisha pointi 49 ikiwa ni pointi 6 mbele ya timu ya Azam inayokamata nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 43.

Kikosi cha Young Africans: 1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Frandk Domayo, 9.Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu, 10.Hamis Kiiza, 11.Nizar Khalfani/Stephano Mwasika

AddThis Social Bookmark Button
Last Updated ( Saturday, 30 March 2013 19:18 )  
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Baada ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya maafande wa jeshi la Mgambo mjini Tanga, timu ya Young Africans... http://t.co/0cGkMCuls4
yanga1935: Timu ya Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Mgambo Shooting ya mjini Tanga katika mchezo... http://t.co/7ixZ5SvQt3
yanga1935: Mpira umemalizika, Mgambo Shooting 1 - 1 Young Africans Msuva dkk 87
yanga1935: Dakika ya 87, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la kusawazisha Mgambo Shooting 1 - 1 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 75, Mgambo Shooting 1 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 61, anaingia Nurdin Bakari anatoka Frank Domayo
yanga1935: Dakika ya 60, Mgambo Shooting 1 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 58, anaingia Haruna Niyonzima anatoka Oscar Joshua
yanga1935: Mwamuzi wa mchezo ameshindwa kuumudu mchezo, anatoa maamuzi ya ajabu ajabu uwanja mzima unamzomea
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Mgambo Shooting 1 - 0 Young Africans
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Mgambo Shooting 1 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 42, Mgambo Shooting wanapata bao la kwanza Mgambo Shooting 1 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 30 , Mgambo Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 15, Mgambo Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Mpira ndio umeanza hapa uwanja wa Mkwakwani kati ya Mgambo Shooting Vs Young Africans
yanga1935: Here's Young Africans line-up to face Mgambo Shooting today: 1.Ally Mustafa 'Barthez' 2.Mbuyu Twite 3.Oscar Joshua... http://t.co/0oP4ElKVYf
yanga1935: Vodacom Premier League 2012/2013 Mgambo Shooting Vs Young Africans Muda : Saa 10 jioni Uwanja : Mkwakwani - Tanga... http://t.co/Pm4huwfisW
yanga1935: Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, timu ya Young Africans leo asubuhi imefanya mazoezi katika uwanja wa... http://t.co/WIjCj0Zhdt
yanga1935: MWENYEKITI wa Kamati ya Uendelezaji wa jengo dogo la Yanga SC, liliopo Mtaa wa Mafia, Kariakoo, Dar es Salaam,... http://t.co/AMKseEwMaj
yanga1935: "sita, saba, nane,tisa, kumi , kumi na sita, kumi na nane, ishirini na tano, ishirini na sita" Hivyo ndivyo... http://t.co/6XoMGy3tzN
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro Cannavaro dkk 5, Msuva dkk 19, Kiiza dkk 43 Yanga imefikisha... http://t.co/wHWqv5IAOB
yanga1935: Dakika ya 78 anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Saimon Msuva
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 3 - 0 jKT Oljoro
yanga1935: Dakika ya 65, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro
yanga1935: Dakika ya 58 Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Said Bahanuzi anatoka Didier Kavumbagu
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro
yanga1935: Dakika ya 43, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao tatu Young Africans 3 - 0 JKT Oljoro
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 2 - 0 JKT Oljoro
yanga1935: Dakika ya 19, Saimon Msuva anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2- 1 JKT Oljoro
AddThis Social Bookmark Button
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday1341
mod_vvisit_counterYesterday1699
mod_vvisit_counterThis week11298
mod_vvisit_counterLast week14133
mod_vvisit_counterThis month40013
mod_vvisit_counterLast month59067
mod_vvisit_counterAll days467585

We have: 28 guests, 1 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Apr 19, 2013