You are here: Home NEWS Local News RIDHIWANI KIKWETE ATEULIWA MWENYEKITI WA UJENZI WA MAFIA

RIDHIWANI KIKWETE ATEULIWA MWENYEKITI WA UJENZI WA MAFIA

E-mail Print PDF

VIEWED 3065 TIMES

Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Sports Club mheshimiwa Yusuf Manji leo amemtambulisha wakili Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi eneo la Ilala jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu Manji amesema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake, na moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga.

"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu, hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta maendeleo ya klabu" alisema Manji

Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.

Mara baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.

"Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani

Aidha Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.

Ridhiwani mwisho alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu.

 

Last Updated ( Thursday, 21 March 2013 17:35 )  

  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara 2012/2013 Young Africans ambao pia ni Mabingwa watetezi wa kombe la Kagame.... http://t.co/1MWhftd8dX
yanga1935: Kilimanjaro Premium Lager – wadhamini wakuu wa timu ya Yanga imetoa kiasi cha shilingi milioni 25 kama zawadi kwa... http://t.co/Jps5DT5SOv
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday991
mod_vvisit_counterYesterday1812
mod_vvisit_counterThis week2803
mod_vvisit_counterLast week14253
mod_vvisit_counterThis month6536
mod_vvisit_counterLast month81178
mod_vvisit_counterAll days578794

We have: 21 guests, 2 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Jun 04, 2013