You are here: Home NEWS Local News YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI

YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI

E-mail Print PDF
VIEWED 313 TIMES
Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi katika katika uwanja wa mabatini Kijitonyama kujiandaa na mchezo namba 135 wa mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom dhidi ya timu ya Toto African siku ya jumamosi Machi 09 ,2013 katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mara baada ya kupata ushindi wa tatu mfululizo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom, kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliendelea na mazoezi katika Uwanja wa mabatini Kijitonyama tangu siku ya jana ikiwa ni maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Toto African.
Young Africans ambayo inapongoza msimamo wa VPL kwa kuwa na pointi 42 na mabao 35 ya kufunga, inahitaji kushinda kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Kuu ya Vodacom ambayo kwa sasa imefikia katika ya mzunguko wa 18.
Katika mchezo wa mwisho Young Africans iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Kagera Sugar bao lililofungwa na kiungo Haruna Niyonzima, tangu mzunguko wa pili uanze Yanga imeshacheza jumla ya michezo mitano na kufanikiwa kushinda michezo minne na kutoka sare mmoja hivyo kujikusanyia point 13 kati ya 15.
Kocha Mkuu Ernest Brandts mara baada ya mazoezi ya leo, amewapa mapumziko wachezaji wake ya siku mbili (jumamosi na jumapili) ili waweze kupata nafasi ya kujumuika na familia zao mwishoni mwa wiki, na mazoezi yataendelea tena siku ya jumatatu asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama.
AddThis Social Bookmark Button
 
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama... http://t.co/rO4zxtgQ2s
yanga1935: Kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeenndelea na mazoezi katika katika uwanja wa mabatini Kijitonyama... http://t.co/SncDl3zN7Y
yanga1935: Bao lililofungwa na kiungo wa kimataifa raia wa Rwanda Haruna Niyonzima dakika ya 66 ya mchezo, limeifanya timu... http://t.co/YdkiR2837a
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 1 - 0 Kagera Sugar Niyonzima dkk 66 Young Africans inazidi kujikita kileleni kwa kufikisha point 42
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 1 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Dakika ya 68, Young Africans inafanya mabadiliko wanaingia Jerson Tegete na Hamis Kiiza kuchukua nafasi za Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi
yanga1935: Dakika ya 66, Haruna Niyonzima anaipatia Young Africans bao la kwanza Young Africans 1 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Dakika ya 45 Didier Kavumbagu anakosa penati, na mpira ni mapumziko Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Dakika ya 45 Didier Kavumbagu anakosa penati
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 Kagera Sugar
yanga1935: Mpira umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Young Africans Vs Kagera Sugar
yanga1935: Here's Young Africans line-up to face Kagera Sugar today: 1.Ally Mustafa 'Barthez' 2.Mbuyu Twite 3.Oscar Joshua... http://t.co/0d4ixgog90
yanga1935: Tukutane Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, majira ya saa 10 za jioni kwa saa za Afrika Mashariki.. http://t.co/QOerDPTaNl
AddThis Social Bookmark Button
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday165
mod_vvisit_counterYesterday1410
mod_vvisit_counterThis week1575
mod_vvisit_counterLast week16146
mod_vvisit_counterThis month9378
mod_vvisit_counterLast month50671
mod_vvisit_counterAll days375815

We have: 4 guests, 3 bots online
Your IP: 207.241.237.102
Mozilla 5.0, 
Today: Mar 06, 2013