You are here: Home NEWS Local News YANGA YAMALIZA MAZOEZI LEO UTURUKI

YANGA YAMALIZA MAZOEZI LEO UTURUKI

E-mail Print PDF
VIEWED 735 TIMES

Timu ya Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.

Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
Akiongelea michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata kisha kupewa penati ya utata pia.
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Last Updated ( Saturday, 12 January 2013 15:41 )  

OUR SPONSORS

  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Young Africans kuivaa Black Leopard ya Afrika Kusini http://t.co/O5qJvtLG
yanga1935: Yanga yawasili Dar salama http://t.co/F8W53VAa
yanga1935: Yanga kutua Dar kesho alfajiri http://t.co/vdElnHqN
yanga1935: Yanga yamaliza mazoezi yake leo kwa kufanya mazoezi ya Gym http://t.co/FPbskpHa
yanga1935: Yanga yapoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya Emmen FC ya Uholanzi, http://t.co/hmfEJOx9
yanga1935: International Friendly Match today: Young Africans Vs Emmen FC Kick-off: 15:00hrs (Turkey) 16:00hrs EAT Venue: Adora Football
yanga1935: Yanga kumaliza na Emmen FC kesho http://t.co/cPoDOREf
yanga1935: Yanga yaendelea kujifua Uturuki http://t.co/l98kqQDj
yanga1935: Yanga 1 - 2 Denizlispor http://t.co/L38pzkUL
yanga1935: Mpira umemalazika, Young Africans 1 - 2 Denizlispor FC Tegete dkk 35 Denizlispor dkk 78,86
yanga1935: Heres Young Africans line-up to face Denizlispor# Barthez,Juma,Kabange,Nadir,Kelvin,Chuji,Msuva,Nurdin,Didier,Kiiza & Niyonzima
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday178
mod_vvisit_counterYesterday2310
mod_vvisit_counterThis week2488
mod_vvisit_counterLast week20239
mod_vvisit_counterThis month42643
mod_vvisit_counterLast month36036
mod_vvisit_counterAll days280875

We have: 10 guests, 2 bots online
Your IP: 207.241.237.238
Mozilla 5.0, 
Today: Jan 16, 2013