You are here: Home NEWS Local News YANGA KWENDA UTURUKI JUMAPILI ALFAJIRI

YANGA KWENDA UTURUKI JUMAPILI ALFAJIRI

E-mail Print PDF

VIEWED 1207 TIMES

Mabingwa mara mbili mfululizo wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki al maarufu(Kagame Cup )timu ya Young Africans inatarajia kuondoka alfajiri ya jumapili kuelekea nchini Uturuki ambako itaweka kambi ya mazoezi kwa muda wa wiki mbili.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, Afisa Habari wa klabu ya Yanga Baraka Kizuguto amesema timu itaondoka alfajiri ya jumapili kwa shirika la ndege la Turkish Airline, ambapo itakua na msafara wa watu 34, wachezaji 27 na viongozi 7.

Timu itaondoka majira ya saa 10:30 alfajiri na itafika katika mji wa Instabul majira ya saa 5 kasoro dakika 10, kisha baadae majira ya saa 9 alasiri itaondoka kwenda katika mji wa Antalya uliopo kusini mwa nchi ya Uturuki ambapo itafika saa 10 ndio haswa itakapokuwa kambi ya timu alisema 'Kizuguto'

Kizuguto amesema timu itafikia katika hotel ya Sueno Beach iliyopo pembezoni mwa bahari ya Meditreanian, na itakua ikifanya mazoezi katika viwanja vikubwa viwili vilivyopo katika hotel hiyo na kiwanja kidogo cha nyasi bandia.

Majina ya watakosafiri keshokutwa alfajri ni:

Walinda Mlango: Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yusuph Abdul

Walinzi wa Pemebeni: Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stephano Mwasika na Oscar Joshua

Walinzi wa kati: Mbuyu Twite, Nadir Haroub, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani

Viungo: Athumani Idd, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari na Omega Seme

Viungo wa Pembeni: Saimon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende

Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerson Tegete, George Banda na Hamis Kiiza

Viongozi watakaoambatana na timu hiyo ni

Kocha Mkuu: Ernest Brandts,

Kocha msaidizi: Fred Felix Minziro,

Kocha wa makipa: Razaki Siwa,

Daktari wa timu: Dr.Suphian Juma,

Meneja wa timu: Hafidh Saleh,

Afisa wa Habari : Baraka Kizuguto

na kiongozi mkuu wa msafara: Mohamed Nyenge ambae ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Yanga

 

 

Last Updated ( Friday, 28 December 2012 12:48 )  
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Yanga yafanya mkutano mkuu wa wanachama salama, ajenda zote zapitishwa http://t.co/lotRChsL
yanga1935: Yanga yaichapa Black Leopard mabao 3-2 http://t.co/8XbabdSs
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 2 Black Leopard Tegete dkk 32,73, Domayo 63 Khoza dkk 47, Rodney dkk 89
yanga1935: Dakika ya 89, Rodney Ramagalela anaipatia Black Leopard bao la pili kwa mkwaju wa penati
yanga1935: Dakika ya 84, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia George Banda anatoka Jerson Tegete
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 3 - 1 Black Leopard anaingia Said Bahanuzi anatoka Didier Kavumbagu
yanga1935: Dakika ya 73, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la tatu Young Africans 3 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 63, Frank Domayo anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 47, Humphrey Khoza anaipatia Black Leopard bao la kusawazisha#Young Africans 1 - 1 Black Leopard
yanga1935: wanaingia Said Mohamed, Saimon Msuva na Juma Abdul Wanatoka Kabange Twite, Mbuyu Twite na Ally Mustafa
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans inafanya mabadiliko wanaingia Said Mohamed, Saimon Msuva na Juma Abdul
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Black Leopard Tegete dkk 32
yanga1935: Dakika ya 32, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 Black Leopard
yanga1935: Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Young Africans Vs Black Leopard
yanga1935: Here's Young Africans line-up to face Black Leopard today#Mustafa,Mbuyu,Oscar,Nadir,Yondani,Chuji,Kabange,Domayo,Didier,Tegete,Niyonzima
yanga1935: International Friendly Match today: #Young Africans Vs Black Leopard Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium
yanga1935: Yanga Vs Black Leopard kesho Taifa http://t.co/o9Uu695M
yanga1935: Yanga yaanza mazoezi baada kurejea kutoka nchini Uturuki http://t.co/WjuE9731
yanga1935: Young Africans kuivaa Black Leopard ya Afrika Kusini http://t.co/O5qJvtLG
yanga1935: Yanga yawasili Dar salama http://t.co/F8W53VAa
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday824
mod_vvisit_counterYesterday2888
mod_vvisit_counterThis week824
mod_vvisit_counterLast week17151
mod_vvisit_counterThis month55150
mod_vvisit_counterLast month36036
mod_vvisit_counterAll days293382

We have: 39 guests, 3 bots online
Your IP: 207.241.237.238
Mozilla 5.0, 
Today: Jan 21, 2013