You are here: Home NEWS Local News YANGA KUWEKA KAMBI UTURUKI, WATATU WAPANDIHSWA KUTOKA U20

YANGA KUWEKA KAMBI UTURUKI, WATATU WAPANDIHSWA KUTOKA U20

E-mail Print PDF
VIEWED 2933 TIMES
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Asalam aleykhum
Habari za muda huu ndugu waandishi wa habari.
Awali ya yote namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa afya njema, pili nawashukuru waandishi wa habari kwa kuitikia mwaliko huu.
Mbele yenu naitwa Abdallah Bin Kleb, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano ya Klabu ya YANGA.
Nimewaita hapa kwa ajili ya kuwaelezea masuala muhimu mawili,
1.Maendeleo ya timu katika ligi kuu ya vodacom
2.Mipango ya kuendelea kufanya vizuri.
Nikianza na suala la kwanza, tangu kuingia madarakani kwa uongozi wetu Julai 15 mwaka huu ni takribani miezi mitano (5), imeshapita, timu ya Yanga imecheza jumla ya michezo 23, imeshinda michezo 19, sare michezo miwili (2), imefungwa michezo mitatu (2).
Timu ya Yanga imefunga jumla ya mabao 52 katika michezo yote, imefungwa mabao 14 katika michezo yote tangu mwezi July 2012.
Timu yetu imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi hiki, ambapo katika mashindano ya Kagame tuliweza kutwaa Ubingwa kwa kuifunga Azam fc katika mchezo wa fainali kwa mabao 2-0, mabao ya Hamis Kiiza na Said Bahaunzi.
Timu ilifikia hatua ya fainali baada ya kushinda michezo 4, dhidi ya Waw Salaam (7-1) APR (2-0) hatua ya makundi, Robo fainali dhidi ya mafunzo (1-1 ) kisha kushinda kwa penati 5-3, na mchezo wa nusu fainali dhidi ya APR kwa ushindi wa bao 1-0
Mpaka kufikia mwisho wa mashindano ya Kagame Yanga ilikuwa imecheza michezo 6, ikishinda michezo mitano (5)na kufungwa mchezo mmoja tu wa ufunguzi (2-0) dhidi ya Athletico Olmypic.
Said Bahanunzi aliibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 6, akifuatiwa na Hamis Kiiza pia wa Yanga aliyefunga mbao 5.
Yanga ilifunga jumla ya mabao 13 katika mashindano ya Kagame na kufungwa mabao 3 tu.
Timu ilikwenda kambi ya mafunzo ya wiki moja nchini Rwanda kufuatia mualiko wa Rais Paul Kagame ambapo ilicheza michezo miwili ya kirafiki na kushinda yote ikiwa ni maandailizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga 2- 0 Rayon Sports
Yanga 2- 1 Police Fc
Baada ya michezo hiyo timu ilirejea nchini tayari kwa ajili ya ligi kwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki, iliyoshinda dhidi ya Moro United (4-0) na Coastal Union (2-1)
Mechi ya kwanza ligi Yanga ilitoka sare (0- 0)dhidi ya timu ya Prisons mjini mbeya, kisha timu ikafungwa mabao 3-0 dhidi ya timu ya mtibwa sugar mjini Morogoro.
Uongozi uliamua kusitisha mkataba na aliyekua kocha mkuu mbeligiji Tom Saintfiet baada ya kutokea kutokuelewana na maagizo ya uongozi,juu ya mila na tamaduni za klabu.
Mholanzi Ernie Brandts aliajiriwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya Yanga kuchukua nafasi ya Tom, na tangu kuwasili kwa Brandts timu imeweza kufanya vizuri kutoka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi kuu iliyoachwa na Tom na kushika nafasi ya kwanza mpaka sasa.
Chini ya Brandts timu imeshinda michezo 7 imetoka sare mchezo 1 na kufungwa mchezo 1 dhidi ya Kagera Sugar, hali inayoashiria uamuzi tuliofanya wa kumleta kocha Brandts umeleta tija kwani timu inacheza soka safi la kuvutia na kuhakikisha tunapata ushindi.
Mpaka sasa tunaongzoa ligi kwa kuwa na pointi 29, tumefunga mabao 25 na kufungwa mabao 10
Huku Azam anayetufuatia akiwa na point 24 ponti tano (5) nyuma yetu.
Didier Kavumbagu anaongoza kwa ufungaji akiwa ameshafunga mabao nane (8) mpaka sasa
Kocha Mkuu Ernie Brandts amewapandisha wachezaji watatu kutoka timu yetu ya vijana ya U-20 baada ya kujiridhisha na uwezo wa wachezaji hao huku pia akiendelea kufuatilia wachezaji wengine katika timu hiyo ya vijana.
Wachezaji waliopandishwa kutoka U-20 ni mshambuliaji George Banda, kiungo wa pembeni Rehani Kibingu na golikipa Yusuph Abdul.
Kikosi cha timu ya vijana tangu mwezi July kimecheza jumla ya michezo 24 ya kirafiki na mashindano, kikiwa imeshinda michezo 20, imetoka sare michezo mitatu (3) na kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya U-20 Ruvu Shooting.
Kupandishwa kwa wachezaji hawa ni ishara tosha kuwa tumeamua kuijenga timu kuanzia kwa timu ya vijana na kwa sasa ikiwa imefika hatua ya robo fainali ya mashindano ya El Talento Soccer Tournament yanayofanyika katika uwanja Etihad Stadium - Mwananyamala.
NB:Ripoti kamili kw ujumla tutaitoa kwenye mkutano mkuu wa wanachama desemba 08, 2012

Suala la pili ni kuhusu mipango ya maandalizi:
Timu imeanza mazoezi rasmi leo asubuhi katika uwanja wa shule ya sekondari Loyola kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kombe la Kagame mwezi januari 2013
Kamati ya mashindano baada ya kukaa na kujadiliana na kocha, kwa pamoja tumeamua timu itakwenda kuweka kambi ya mafunzo nchini Uturuki kwa kipindi cha wiki mbili, safari ya Uturuki itakua ni mara tu baada ya sikukuu ya X-mass kabla ya mwaka mpya.
Hii itatoa fursa kwa wachezaji wote kuweza kujumuika pamoja kwani kwa sasa baadhi ya wachezaji wetu wapo wanazitumikia timu zao za taifa kwenye mashindano ya Chalenji nchini Uganda.
Hivyo mara tu mashindano ya Chalenji yatakapomalizika, watarejea nchini kujiunga na mazoezi na wachezaji wenzao tayari kujiandaa na safari hyo ya Uturuki.
Tumeamua kuipeleka timu kambini nchini Uturuki kufuatia mapendekezo ya kocha mkuu, kwani kuna huduma bora zaidi kwa ajili ya kambi.
Kocha ana uzoefu na nchi ya Uturuki hivyo alivyotueletea mapendekezo yake ya kupeleka timu, tulimkubalia na kuanza kuandaa maandalizi ya kambi hiyo lengo ikiwa ni kuifanya timu ya Yanga kucheza soka safi la burudani na kupata ushindi.
Timu ikiwa kambi nchini Uturuki itapata nafasi ya kufanya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu na mashindano ya Kagame yanayotegemewa kufanyika mwezi januari mwakani, kulingana na kambi hiyo ya Uturuki wachezaji na benchi la ufundi watapata huduma zote zinazohusiana na kambi.
Timu ikiwa nchini Uturuki inatazamiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu mbili ambazo zitajulikana baadae na tutawajulisha kabla ya kuondoka.
Kocha Brandts anaangalia sana Nidhamu ndani na nje ya uwanja, kwani anaamini nidhamu ndio msingi wa timu kufanya vizuri.
Pili ni kocha anapenda kila mchezaji awe na malengo, na si kucheza mpira tu pasipokuwa na malengo,
Lazima mchezaji ajue kabla ya kuwaza kucheza soka nje ya nchi inampasa kupigania kuhakikisha anapata namba katika kikosi cha kwanza cha timu yake.
Pia kocha anaamini wachezaji wakiishi kwa upendo pasipo kuchukiana kutaifanya timu kuendelea kuwa katika hali nzuri na kucheza mpira kwa bidii na kujituma kufikia mafanikio.
Kuhusu Usajili kocha ametuletea mapendekezo yake, tunayafanyia kazi na muda ukiwa tayari tutawajulisha, maana dirisha dogo la usajili linafungwa disemba 15 hivyo bado tuna siku zaidi ya 20.
Hatupendi masuala ya kukurupuka kutangaza vitu ambavyo havijakalmilika, ndio maana hata usajili wetu uliopita tulitangaza baada ya kukamilisha kila kitu.
Hayo ndo machache niliyotaka kuwajulisha ndugu zangu waandishi wa habari.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Abdallah Bin Kleb
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano na usajili
Last Updated ( Tuesday, 18 December 2012 10:07 )  
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: Yanga yafanya mkutano mkuu wa wanachama salama, ajenda zote zapitishwa http://t.co/lotRChsL
yanga1935: Yanga yaichapa Black Leopard mabao 3-2 http://t.co/8XbabdSs
yanga1935: Mpira umemalizika, Young Africans 3 - 2 Black Leopard Tegete dkk 32,73, Domayo 63 Khoza dkk 47, Rodney dkk 89
yanga1935: Dakika ya 89, Rodney Ramagalela anaipatia Black Leopard bao la pili kwa mkwaju wa penati
yanga1935: Dakika ya 84, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia George Banda anatoka Jerson Tegete
yanga1935: Dakika ya 75, Young Africans 3 - 1 Black Leopard anaingia Said Bahanuzi anatoka Didier Kavumbagu
yanga1935: Dakika ya 73, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la tatu Young Africans 3 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 63, Frank Domayo anaipatia Young Africans bao la pili Young Africans 2 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 60, Young Africans 1 - 1 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 47, Humphrey Khoza anaipatia Black Leopard bao la kusawazisha#Young Africans 1 - 1 Black Leopard
yanga1935: wanaingia Said Mohamed, Saimon Msuva na Juma Abdul Wanatoka Kabange Twite, Mbuyu Twite na Ally Mustafa
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Young Africans inafanya mabadiliko wanaingia Said Mohamed, Saimon Msuva na Juma Abdul
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Black Leopard Tegete dkk 32
yanga1935: Dakika ya 32, Jerson Tegete anaipatia Young Africans bao la kwanza kwa mkwaju wa penati
yanga1935: Dakika ya 30, Young Africans 0 - 0 Black Leopard
yanga1935: Dakika ya 15, Young Africans 0 - 0 Black Leopard
yanga1935: Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Young Africans Vs Black Leopard
yanga1935: Here's Young Africans line-up to face Black Leopard today#Mustafa,Mbuyu,Oscar,Nadir,Yondani,Chuji,Kabange,Domayo,Didier,Tegete,Niyonzima
yanga1935: International Friendly Match today: #Young Africans Vs Black Leopard Kick-off 16:00hrs Venue: National Stadium
yanga1935: Yanga Vs Black Leopard kesho Taifa http://t.co/o9Uu695M
yanga1935: Yanga yaanza mazoezi baada kurejea kutoka nchini Uturuki http://t.co/WjuE9731
yanga1935: Young Africans kuivaa Black Leopard ya Afrika Kusini http://t.co/O5qJvtLG
yanga1935: Yanga yawasili Dar salama http://t.co/F8W53VAa
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday826
mod_vvisit_counterYesterday2888
mod_vvisit_counterThis week826
mod_vvisit_counterLast week17151
mod_vvisit_counterThis month55152
mod_vvisit_counterLast month36036
mod_vvisit_counterAll days293384

We have: 40 guests, 3 bots online
Your IP: 207.241.237.238
Mozilla 5.0, 
Today: Jan 21, 2013