VIEWED 481 TIMES

Timu ya Young Africans Sports Club kesho jumamosi, itashuka dimbani kucheza dhidi ya timu ya JKT Oljoro FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kikosi cha wachezaji 20 na benchi la Ufundi 7 kiliwasili salama jana jioni majira ya saa 11, na majira ya saa 12 jioni kilifanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
Young Africans itaingia uwanjani kwa lengo la kusaka pointi 3 muhimu ambazo zinaweza kuipelekea kuongoza Ligi katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom endapo mchezo kati ya Simba na Azam ziatatoka sare, na kama Azam au Simba mmoja akishinda na Yanga ikashinda basi itakwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo.
Kochaa mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema anashukru vijana wake wote vizuri na wamefika salama na hakuna mchezaji majeruhi katika wachezaji waliopo Arusha hivyo anaamini timu yake itaibuka na ushindi.
Katika mchezo wa mwisho dhidi ya Polisi Morogoro Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam , Young Africans iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, shukrani kwa mabao ya Saimon Msuva, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza.
Kikosi kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo jioni majira ya 10, yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mpambano hapo kesho.
Wachezaji waliopo Arusha ni:
Walinda Mlango: Yaw Berko, Ally Mustapha 'Barthez'
Walinzi wa Pembeni: Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, David Luhende,
Walinzi wa Kati: Kelvin Yondani, Mbuyu Twite, Ladisalus Mbogo, Nadir Haroub 'Cannavaro'
Viungo Wakabaji: Frank Domayo, Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif 'kijiko'
Viungo Washambuliaji: Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo, Nurdin Bakari
Washambuliaji: Saimon Msuva, Nizar Khaflan, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Jeryson Tegete














