You are here: Home NEWS Local News WAZEE WATOA TAMKO, JUU YA NEMBO YA VODACOM

WAZEE WATOA TAMKO, JUU YA NEMBO YA VODACOM

E-mail Print PDF

VIEWED 1973 TIMES

Katibu wa Baraza la wazee wa klabu ya Young Africans Sports Club, Mzee Ibrahim Akilimali ametoa ufafanuzi juu ya timu ya Yanga kutovaa jezi zenye nembo nyekundu ya mdhamini wa ligi kuu Tanzania bara kampuni ya simu ya Vodacom.

Akiongea na wandishi wa habari makao makuu ya klabu makutano ya mitaa ya Twiga/Jangwani, Mzee Akilimali amesema kamwe hawatakubali matakwa ya vodacom na TFF ya kuweka nembo yenye doa jekundu katika jezi za Yanga.

Ni afadhali hao TFF watufute katika ligi yao kama wataendelea kutulazimisha kuvaa jezi zenye nembo nyekundu, kwani tupo radhi kubaki kucheza michezo isiyodhaminiwa na Vodacom kama bao, ngumi, na mingineyo au hata kuhamia ligi ya visiwani Zanzibar ambako tutacheza bila vikwazo.

Labda kwa wasiofahamhu historia, Yanga mwaka 1953 mbele ya aliyekua Gavana wa Tanganyika, Sir Edward Twinning ilikataa kuvaa jezi zenye madoa ya rangi nyekundu ilizoletewa na timu pinzani ya mabaharia kutoka Uingereza, na kusema ni bora tucheze vifua wazi kuliko kuvaa jezi hizo alisema 'Mzee Akilimali'.

Mzee Akilimali aliongeza pia kuwa hata chama cha TANU kiliwahi kuiomba Yanga ibadilishe rangi zake za kijani na njano, lakini Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa Julius Nyerere aliwambia wajumbe wa TANU kwamba waacheni Yanga na rangi zao, rangi hizo wanazotumia zinawatambulisha wao, madini, na maliasili ya nchi hii.

Aidha pia Mzee Akilimali alisema mnamo mwaka 1963, aliyekuwa mkuu wa mkoa Dar es salaam mh Mustapha Songambele aliziita timu zote zilizokuwa na majina ya kigeni kwamba zibadilsihe majina hayo na kujiita majina ya kitanzania, timu zote zilibadilisha majina lakini Young Africans ilipotafsiriwa ilileta maana ya Vijana wa Afrika hali iliypolekea Yanga kuendelea kutumia jina lake, na timu zingine kubadilisha majina yao.

Kaimu katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema wanashindwa kuelewa kwa nini vodacom mwaka huu wanalazimisha Yanga ivae jezi zenye rangi jekundu, ili hali mwaka jana walikubali kutoa jezi zenye rangi nyeusi ya doa la vodacom.

Mkataba kati ya TFF na Vodacom sisi hatujauona, sasa inakuwa vigumu kujua kipi kimeandikwa ndani ya huo mkataba na kinapaswa kutekelezwa, ilipaswa vilabu tuepewe nakala ya mkataba tuusome kabla ya kusainiwa, ili na sisi tupate nafasi ya kutoa hoja katika mkataba huo, lakini wao wamefanya kinyume kisha wanatulazimisha tuvae hiyo nembo, ikiwa hatujui maslahi ya mkataba wenyewe alisema 'Mwalusako'.

Yanga itashuka dimbani siku ya jumamosi kucheza na timu ya Ruvu Shooting katika muendelezo wa michezo ya Ligi ya Kuu ya Vodaco nchini raundi ya 8.

Naye Mzee Mwika aliongezea kwa kutoa mfano kwamba "haiwezekani Mnyamwezi aje zake Pwani toka Tabora atukataze wazaramo kucheza mdundiko au dogoli", alichokikuta anapaswa kukifuata na kukiheshimu na sio kuja na kutaka kubadillisha tamaduni za watu, Yanga ina rangi kuu tatu (3) Kijani, Njano na Nyeusi.

 

 

AddThis Social Bookmark Button
Last Updated ( Wednesday, 17 October 2012 16:15 )  
  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

yanga1935: I posted 12 photos on Facebook in the album "Mazishi ya Hamza Said (Zola)" http://t.co/c03XqvTBUK
yanga1935: Mamia ya wanachama, wapenzi na mashabiki wa soka leo jioni wameshiriki katika safari ya mwisho ya kuusindikiza... http://t.co/j9a41B4NIH
yanga1935: Aliyekuwa mfanyakazi wa klabu ya Yanga katika idara ya utumishi (sekretarieti) Hamza Said al maarufu kama Zola au... http://t.co/ISNtyXGIRb
yanga1935: Hamza Said (Zola, Chiluba) amefariki leo alfajiri kwa ajali ya kugongwa na gari. Zola alikuwa mfanyakazi wa Yanga SC http://t.co/DdbGYuqnRH
yanga1935: TANZIA: Uongozi wa klabu ya Yanga unasikitika kutangaza kifo cha mfanyakazi Hamza Said almaarufu kama Zola au... http://t.co/ZWs9NdGmqe
yanga1935: "Pisha pisha Yanga inapita, Pisha Njia Yanga inapita, Pisha pisha Mabingwa wanapita" Hivyo ndivyo washabiki,... http://t.co/QOJDmCM8ys
yanga1935: Mpira umemalizika, Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans Kiiza dkk 48
yanga1935: Dakika ya 80, Young Africans inafanya mabadiliko anaingia Didier Kavumbagu kuchukua nafasi ya Nizar Khalfani aliyeumia
yanga1935: Dakika ya 75, Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 60, Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 48, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza Ruvu Shooting 0 - 1 Young Africans
yanga1935: Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Mpira ni mapumziko, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 30, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Dakika ya 15, Ruvu Shooting 0 - 0 Young Africans
yanga1935: Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Ruvu Shooting Vs Young Africans
yanga1935: Here's Young Africans line-up to face Ruvu Shooting today: 1.Ally Mustafa 'Barthez' 2.Juma Abdul 3.Oscar Joshua... http://t.co/IFGj2qf2q5
yanga1935: Saturday Vodacom Premier League 2012/2013 Young Africans Vs Ruvu Shooting Venue: National Stadium Time: 16:00hrs... http://t.co/KtXaFTlNDD
yanga1935: I posted 2 photos on Facebook in the album "Yanga SC wakisoma Dua" http://t.co/dvBpNuoXeA
yanga1935: Ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kwa kuwa na pointi 45, timu ya Young Africans kesho itashuka... http://t.co/gL3YKmmsON
yanga1935: Mlinzi wa kati wa timu ya Young Africans Ladislaus Mbogo anaendelea vizuri baada ya jana kufanyiwa upasuaji wa... http://t.co/1rcHnFSUZ6
yanga1935: Timu ya Young Africans leo imeingia kambini katika hosteli zilizopo makao makuu ya klabu mitaa ya Twiga/Jangwnai... http://t.co/AWJwjt4Dud
AddThis Social Bookmark Button
mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday929
mod_vvisit_counterYesterday2319
mod_vvisit_counterThis week3248
mod_vvisit_counterLast week14464
mod_vvisit_counterThis month36334
mod_vvisit_counterLast month50671
mod_vvisit_counterAll days402771

We have: 24 guests, 3 bots online
Your IP: 207.241.237.238
Mozilla 5.0, 
Today: Mar 19, 2013