You are here: Home NEWS Local News NUSU FAINALI KAGAME 2012, YANGA Vs APR, AZAM Vs AS VITA

NUSU FAINALI KAGAME 2012, YANGA Vs APR, AZAM Vs AS VITA

E-mail Print PDF

2012-07-25 15:07:18 VIEWED 394 TIMES

Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu Kombe la Kagame 2012, yamefikia hatua ya Nusu Fainali ambapo timu nne(4) zitachuana siku ya alhamis kusaka timu timu mbili ambazo zitacheza fainali siku ya jumamosi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 

 

Mabingwa watetezi wa kombe hilo klabu ya Young Africans itashuka dimbani kucheza na tim ya APR kutoka Rwanda katika nusu fainali ya pili itakayofanyika jioni majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Nusu Fainali ya kwanza itaanza majira ya saa 8:00 mchana kwa kuzikutanisha timu za Azam FC (Tanzania) na timu ya AS Vita ya (DRC), timu ya Azam imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya Simba SC ya Tanzania pia kwa jumla ya mabao 3-1.

AS Vita nayo imefanikiwa kufika hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Atletico FC ya nchini Burundi kwa mabao 2-1 katika mchezo uliochzwa hapo awali.

Young Africans iimefanikiwa kufika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penati 5-3, kufuatia kumalizika kwa dakika 90, ztimu zote zikiwa sare ya mabao 1-1.

APR kutoka Rwanda iliifinga timu ya URA kutok Uganda mabao 2-0 katika mchezo wa robo fainali na hivyo kupata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.

Kocha mkuu wa Young Africans Tom Saintfiet akiongea na tovuti ya klabu wwww.youngafricans.co.tz alisema anajua mchezo dhidi ya APR ni mgumu, kwani mchezo wa kwanza tulishinda kwa mabao 2-0, hivyo naamini APR wataingia Uwanjani wakiwa na nia ya kusaka ushindi tu ili waweze kucheza hatua ya fainali.

Saintfiet pia alisema pamoja na kuwa na mchezo huo mgumu dhidi ya APR, anaamin vijana wake wako katika hali nzuri ya ushindi, na maandalizi yote ya mchezo yamekamilika, hivyo anaamini timu yake Young Africans itaibuka na ushindi katika mchezo huo.

Mungu Ibariki Young Africans, Mungu Ibariki Tanzania.

'YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO'

Last Updated ( Wednesday, 25 July 2012 12:45 )  

OUR SPONSORS

  • FACEBOOK PAGE

  • TWITTER FEEDS

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday27
mod_vvisit_counterYesterday1181
mod_vvisit_counterThis week2375
mod_vvisit_counterLast week8050
mod_vvisit_counterThis month9547
mod_vvisit_counterLast month27959
mod_vvisit_counterAll days83298

We have: 6 guests, 2 bots online
Your IP: 204.236.235.245
 , 
Today: Aug 09, 2012