2012-04-13 09:35:44 VIEWED 137 TIMES
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Sports Club, Wakili Theonist Rutashoborwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospital ya Agha Khan alipokuwa amepelekewa usiku huo mara baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
Rutashoborwa alikuwa mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Young Africans toka mwaka 2010, akiingia katika kamati hiyo iliyoingia madarakani katika uchaguzi mkuu wa klabu chini ya uongozi wa Mwenyekiti Llyod Nchunga.
Marehemu amefariki ghafla jana usiku, ikiwa ni mda mchache toka afike uwanja wa ndege wa Mwl.JK Nyerere akitokea Kilimanajaro ambapo siku mbili zilizopita alikuwa jijini Mwanza pia kwa shughuli zake za kikazi za uanasheria.
Msemaji wa familia ya marehemu amesema kuwa mara baada ya kufika uwanja wa ndege wa KIA jana alianza kujisikia vibaya na kulalamika kuishia nguvu hivyo mara baada ya kufika uwanja wa ndege JK Nyerere alikimbizwa moja moja hospital ya Agha Khan, ambapo mauti ilimfika.
Marehemu alishiriki kikamilifu shughuli zote za kamati ya utendaji na klabu kwa ujumla, na mara ya mwisho alikuwepo jijini Tanga na timu ya Young Africans wiki mbili zilizopita katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya wenyeji Coastal Union na Young Africans.
Marehemu ataagwa jumatatu katika kanisa Katoliki parokia ya Kijichi, na jioni mwili wa marehemu utasafirishwa kuelekea mjini Bukoba, mazishi yatafanyika siku ya jumatano katika kijiji cha Bukayaba kilomita 22 kutoka Buko mjini.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amen!
Bwana ametoa na Bwana ametwaa!














