You are here: Home NEWS International News CHELSEA 1 BARCELONA 0

CHELSEA 1 BARCELONA 0

E-mail Print PDF
2012-04-19 12:56:33 VIEWED 746 TIMES
Didier Drogba aliishangaza Barcelona alipofunga bao la Chelsea, na la pekee, katika mechi dhidi ya Barcelona, na kuiongezea timu yake matumaini ya kufika katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.
Drogba alifunga katika kipindi cha kwanza, baada ya dakika mbili kuongezwa, huku vijana wa meneja wa Chelsea, Roberto di Matteo wakiimarisha ngome kali katika uwanja wao wa Stamford Bridge.
Barcelona waliumiliki mpira daima katika mechi hiyo, lakini walishindwa kumpita kipa wa Chelsea, Petr Cech.
Mara mbili Barcelona waligonga mwamba, lakini kweli bahati haikuwa yao.
Hayo yalimpata Alexis Sanchez katika kipindi cha kwanza, na baadaye naye Pedro akitumaini kufunga bao la chini kwa chini, hakufanikiwa, na baadaye mkwaju wake pia ukigonga mwamba.
Kiungo cha kati wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, naye alielekea kufunga, lakini mpira ukaokolewa na Ashley Cole kabla tu ya kuingia wavuni.
Ingawa Chelsea imefanikiwa kuongoza mkondo wa kwanza wa nusu fainali baada ya timu hizo kukutana Jumatano jioni, bila shaka wachezaji hao wa timu ya England wanafahamu watakuwa na kibarua kigumu katika uwanja wa Nou Camp wiki ijayo katika mkondo wa pili
 

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER

mod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_countermod_vvisit_counter
mod_vvisit_counterToday3365
mod_vvisit_counterYesterday11260
mod_vvisit_counterThis week26945
mod_vvisit_counterLast week36083
mod_vvisit_counterThis month77944
mod_vvisit_counterLast month188334
mod_vvisit_counterAll days1466667

We have: 113 guests, 5 bots online
Your IP: 207.241.237.222
Mozilla 5.0, 
Today: Feb 14, 2014