VIEWED 1068 TIMES
Mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu wa 2012/2013 timu ya Young Africans leo imetoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya timu ya Coastal Union (wagosi wa kaya) kutoka jijini Tanga katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo mara baada ya mchezo wa leo, imefikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kufuatia kutangazwa mabingwa tangu mwishoni mwa wiki baada ya timu ya Azam FC kutoka sare ya bao 1-1 na wagosi wa kaya Coastal Union.
Kocha Mkuu Ernie Brandts aliwaongoza wachezaji kuingia uwanjani kwa kuwapungia mikono washabiki wa Yanga nusu ya uwanja hali iliyofawafanya wapenzi, washabiki na wanachama kufurahishwa na kitendo hicho ambacho walijisikia furaha sana.
Katika mchezo wa leo, Brandts aliwapumzisha wachezaji sita wa kikosi cha kwanza ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kupata nafasi ya kucheza na kuonyesha uwezo wao katika mchezo wa leo.
Dakika ya 3 ya mchezo, mshambuliaji Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza kufuatia kuwatoka walinzi wa Coastal Union na kumpiga chenga mlinda mlango Shaban Hassan 'Kado' na kuukwamisha mpira wavuni.
Yanga iliendelea kulishambulia lango la Coastal Union lakinji kutokua makini kwa washambuliaji wake Jerson Tegete, Said Bahanuzi, Nizar Khalfani na Abdallah Mnguli kuliifanya Yanga kukosa mabao ya wazi.
Dakika ya 16 ya mchezo kiungo wa timu ya Coastal Union Abdi Banda aliipatia timu yake bao la kusawazisha kufuatia mpira wa faulo alioupiga kumshinda mlinda mlango Said Mohamed na kujaa moja moja kwa wavuni na kuhesabu bao la kusawazisha.
Timu zote ziliendelea kushambuliana dakika 90 zote za mchezo lakini hakuna timu iliyopata bao lolote.
Mara baada ya mchezo kocha Mkuu wa Brandts amesema kikosi chake kimekosa ushindi kufuatia wachezaji kucheza na kutojituma kutokana na kuingia uwanjani na mawazo ya kutangazwa mabingwa kabla ya ligi kumalizika.
Wachezaji walicheza kwa kutokua makini na hasa sehemu ya kiungo haikuwa vizuri, nadhani imetokana na wachezaji wangu kuingia uwanjani na mawazo ya kuwa tayari mabingwa hicho ndo kilichochangia kutopata ushindi katika mchezo wa leo.
Kivutio kikubwa katika mchezo huo ilikuwa ni kwa washabiki wa Yanga ambao walijitokeza na makombe yao ya bandia nakushangilia tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho huku wengine wakiwa wameandaa kombe kubwa la mbao ambalo liliweka sahihi na wachezaji wote na benchi la ufundi.
Young Africans: 1.Said Mohamed, 2.Mbuyu Twite, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub, 5.Kelvin Yondani, 6.Nurdin Bakari, 7.Nizar Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Said Bahanuzi/George Banda, 10.Jerson Tegete, 11.Abdallha Mnguli/Haruna Niyonzima





















