You are here: Home

The Official Website of Young Africans Sports Club

MALINZI MGENI RASMI MKUTANO MKUU TFF

2012-04-20 13:06:08 VIEWED 762 TIMES
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili (Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es Salaam.
Read more...
 

RUTASHOBORWA AFARIKI DUNIA

2012-04-13 09:35:44 VIEWED 962 TIMES

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Young Africans Sports Club, Wakili Theonist Rutashoborwa amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospital ya Agha Khan alipokuwa amepelekewa usiku huo mara baada ya kuzidiwa na ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.
Read more...
 

YANGA YAELEKEA MWANZA, KUIVAA TOTO AFRICANS JUMAPILI

2012-04-11 08:45:23 VIEWED 929 TIMES
Kikosi cha Mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ambao pia ni mabingwa wa ligi kuu nchini timu ya Young Africans kimeondoka alfajiri ya leo kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya kucheza mchezo wake wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania bara nchini dhidi ya timu ya Toto Africans, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Read more...
   

YANGA WALITEKA JIJI LA TANGA

2012-03-30 13:21:44 VIEWED 986 TIMES

Kikosi cha Mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati na ligi kuu nchini Tanzania bara, Young Africans imeliteka jiji la Tanga na viunga vyake mara baada ya kuwasili humo, huku wenyeji wa jiji hilo wakiwa na hamu na shauku ya kuwaona mabingwa hao waliotua hapa kwa ajili kusaka pointi 3 muhimu ambazo zitawarudisha katika nafasi ya pili ya msimao wa ligi kuu ya Vodacom.

Read more...
 

KIIZA AMFUNGA MDOMO JULIO

2012-03-31 20:06:17 VIEWED 991 TIMES
Bao lililofungwa na mchezaji wa kimataifa kutoka uganda Hamis Kiiza dakika ya 85, limetosha kuipa ushindi timu ya Young Africans Sports Club dhidi ya wenyeji timu ya Coastal katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania bara, mchezo uliochezwa katika dimba la mkwakwani jijini Tanga, kuwacha midomo kimya washabiki wa timu hiyo na kocha mkuu Julio wasijue cha kusema
Read more...
   

Page 71 of 80

  • FACEBOOK

  • TWITTER