";} /*B6D1B1EE*/ ?>
You are here: Home LIBRARY OLD NEWS PAPERS

OLD NEWS PAPERS

OLD NEWS PAPERS:

Library

MJUE KITWANA MANARA

2012-02-23 12:00:19 VIEWED 3093 TIMES

Mjue Kitwana Manara Popat aliyeiletea mafanikio Yanga katika mashindano mbalimbali.

Kitwana Manara maarufu kama ( POPAT ) ni mchezaji ambaye hata sahaurika katika rekodi ya wachezaji waliowahi kuichezea Klabu ya Yanga katika miaka ya 60 hadi 80

Alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga walioiwezesha timu hiyo kuwa ya kwanza nchini kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika mara mbili, 1969 na 1970.

Katika hatua zote hizo mbili, Yanga ilitolewa na Asante Kotoko ya Ghana, ambapo katika robo fainali ya mwaka 1969, iliondoshwa kwa njia ya kura ya shilingi baada ya matokeo ya jumla kuwa sare ya bao 1-1.

Katika robo fainali ya pili mwaka 1970, Yanga ilikutana tena na Asante Kotoko, ambapo katika mechi ya awali, zilitoka sare ya bao 1-1 na katika mechi ya marudiano, hazikufungana.

Mshindi wa pambano hilo ilibidi apatikane katika muda wa nyongeza, lakini kutokana na giza kutanda uwanjani, mechi ilivunjika dakika ya 19 na hivyo kuhamishiwa kwenye uwanja huru wa mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Katika mechi hiyo ya tatu, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Asante Kotoko na kutolewa kwenye hatua hiyo. Kikosi cha Yanga wakati huo kilikuwa chini ya Victor Stanculescu kutoka Romania.

Manara pia alikuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Taifa Stars kufuzu kucheza

michezo ya All Africa Games mwaka 1973 na kutinga nusu fainali, ambapo ilitolewa na Algeria baada ya kuchapwa mabao 2-1.

Last Updated on Thursday, 23 February 2012 09:27

Read more...

 

  • FACEBOOK

  • TWITTER