David Beckham apinga kauli ya Blatter.
Article hits: 2201 Views.
Kiungo wa kimataifa ambaye pia aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya England David amesema taarifa iliyotolewa na rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter juu ya ubaguzi wa rangi kuwa haupo uwanjani linahitaji kutolewa ufafanuzi.
Beckham ambaye sasa ameamea kusakata soka barani ulaya baada ya kuitumikia klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani kwa kipindi cha miaka mitano amesema kauli iliyotolewa na bosi wa FIFA siyo ya kufurahisha.
“Nafikiri kauli iliyotolewa Sepp Blatter juu ya ubaguzi wa rangi inahitaji kupingwa” alisema nahodha huyo wa zamani David Bekham.
