You are here: Home NEWS Local News

Local News

News

YANGA YAMSHITAKI OKWI

Klabu ya Young Africans imemshitaki mchezaji Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka mwili.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa ya Twiga/Jangwani, mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf Manji amesema wameshangazwa na kitendo hicho kilichofanywa na viongozi wa Simba , wakala wake na mchezaji mwenyewe.

"Emmanuel Okwi awali tulishapeleka malalamiko TFF na kuwapa nakala CAF na FIFA juu ya kufanya mazungumzo na timu ya Wadi Degla FC ya nchini Misri na kufikia klabu hiyo kutuma ofa ya kutaka kumnunua bila kuwasiliana na uongozi wetu" alisema Yusuf.

Ikiwa hilo tunasubiria majibu kutoka TFF jana mchezaji huyo amesaini mkataba mwingine, hii inaonyesha ni jinsi gani mchezaji huyu kuna watu walikua wanamrubuni,kwa kusaini mkataba mwingine kitu ambacho amekiuka sheria za FIFA za usajili.

Baada ya kuona jana amesaini mkataba na Simba, Yanga tulichokifanya leo ni kuandika barua nyingine TFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa fidia ya US Dollar 500,000 (sawa na TZS 800,000,000/=) kutoka kwa klabu ya Simba, wakala wake na mchezaji mwenyewe aliongeza "Manji"

Aidha uongozi wa Yanga umeiomba TFF kuwa imelipatia ufumbuzi suala hilo ndani ya siku saba, na kama siku saba zikikpita basi uongozi wa Yanga utakwenda moja kwa moja FIFA na ikishindakana mahakama ya soka CAS.

Lengo sio kuikomoa timu ya Simba, bali tunachotaka ni sheria ifuatwe, Okwi alikua ameitumikia klabu ya Ynaga kwa kipindi cha miezi sita tu, na kuwa amebakiza mkataba wa miaka miwili mpaka msimu mwishoni mwa msimu wa 2015/2016.

Mchezaji anayekutwa na kosa la kusaini sehem mbili adhabu yake ni kufungiwa kucheza soka kuanzia mwaka mmoja na kuendelea huku klabu husika ikifungiwa kusajili kuanzia miaka mwili na kuendela na kushushwa daraja au adhabu zote kwa pamoja.

 

 

 

News

YANGA YAMSHITAKI OKWI

VIEWED 8935 TIMES

Klabu ya Young Africans imemshitaki mchezaji Emmanuel Okwi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili.

Last Updated on Friday, 29 August 2014 14:44

Read more...

 

News

YANGA YATUA PEMBA

VIEWED 5185 TIMES

Msafara wa watu 35 ukiwa na wachezaji 27 na benchi la Ufundi 8 wa timu ya Young Africans tayari umeshawasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.

Last Updated on Monday, 18 August 2014 08:37

Read more...

   

News

EDWARD CHARLES ASAINI MIWILI

VIEWED 4952 TIMES

Mlinzi wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Edward Charles Manyama kutoka timu ya JKT Ruvu Stars leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2) tayari kwa kuitumikia timu ya Young Africans SC kuanzia msimu huu wa 2014/2015.

Last Updated on Tuesday, 19 August 2014 07:08

Read more...

 

News

KIULA KUZIKWA LEO

VIEWED 2162 TIMES

Aliyekuwa Dereva wa Bus kubwa la wachezaji wa klabu ya Young Africans Bw Maulid Kiula anatarajiwa kuzikwa leo mchana katika eneo la Kibaha, baada ya kuagwa asubuhi na wachezaji, viongozi pamoja na wanachama katika Hospital ya Amana Ilala jijini Dar es salaam.

Last Updated on Wednesday, 13 August 2014 11:29

Read more...

   

  • FACEBOOK

  • TWITTER