YANGA YAICHAPA STAND UTD 3-0
Sat - 25 Oct
Written by Administrator
Young Africans imewachapa wenyeji timu ya Stand United kwa mabao 3-0, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliofanyika jioni ya leo katika Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, huku mshambulaji Jerson Tegete akibuka mchezaji bora wa mchezo kwa kukwaisha wavuni mabao mawili peke yake.
Kocha Marcio Maximo leo alibadilisha mfumo kwa Haruna Niyonzima kucheza zaidi pembeni, na kiungo Andrey Coutinho kucheza dimba la juu hali iliyopelekea timu kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Stand United,
Dakika ya 12 ya mchezo, mshambuliaji raia wa Brazil Geilson Santana "Jaja" aliwainua vitini mashabiki waliojitokeza uwanjani kwa kuipatia timu yake bao la kwanza akimalizia pasi nzuri ya kiungo Andrey Coutinho.
Mara baada ya bao hilo wenyeji Stand walicharuka na kusaka bao la kusawazisha lakini umakini wa walinzi wa Yanga walikua kikwazo kwao, na kujikuta wakishambulia bila mafanikio.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha pili cha kwanza zinamalizika, Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1- 0.
Kipindi cha pili cha mchezo kilianza kwa Young Africans kufanya mabadiliko ambapo waliingia Hussein Javu na Jerson Tegete kuchukua nafasi za Andrey Coutinho na Geilson Santana "Jaja" mabadiliko yaliyosaidia na kubadilisha hali ya mchezo.
Dakika ya 78 ya mchezo, mshambuliaji Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la pili la mchezo kwa kumchambua mlianda mlango wa Stand United baada ya kupenyezewa pasi safi na Hussein Javu.
Huku watu wakiwa wameanza kutoka Uwanjani wakifiri mchezo umemalizika, Jerson Tegete tena aliipatia Young Africans bao la tatu na la ushindi baada ya kupokea pasi ya Hassan Dilunga aliyewatoka walinzi wa Stand United na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 - 0 Stand United.
Mara baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo aliwapongeza wachezaji wake kwa kazi nzuri waliofanya na kusema maandalizi dhidi ya Kagera Suagr yanaanza mara moja.
Young Africans: 1.Deo Munish "Dida", 2. Juma Abdul, 3. Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6. Mbuyu Twite, 7. Hassan Dilunga, 8. Coutinho, 9. Jaja/Tegete, 10.Mrisho Ngasa, 11.Haruna Niyonzima/Nizar