You are here: Home NEWS Local News EDWARD CHARLES ASAINI MIWILI

EDWARD CHARLES ASAINI MIWILI

E-mail Print PDF

VIEWED 3881 TIMES

Mlinzi wa kushoto wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Edward Charles Manyama kutoka timu ya JKT Ruvu Stars leo amesaini mkataba wa miaka miwili (2) tayari kwa kuitumikia timu ya Young Africans SC kuanzia msimu huu wa 2014/2015.

Edward Charles Manyama beki wa kushoto wa timu ya Taifa Tanzania amekamilisha taratibu zote kutoka katika timu yake ya JKT Ruvu leo mchana na sasa kuanzia kesho ataonekana katika mazoezi ya kikosi cha kocha mkuu Marcio Maximo tayari kwa mikikimikiki ya VPL msimu huu.

Usajili wa Manyama unafanya idadi ya wachezaji wapya msimu huu kufikia watano (5) wakiwemo washambuliaji wabrazil Andrey Coutinho, Geilson Santos "Jaja", Kiungo mkabaji Said Juma "Makapu" na mlinzi wa kati Pato Ngonyani.

 

 

Last Updated ( Tuesday, 19 August 2014 07:08 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER