You are here: Home NEWS Local News YANGA 1- 1 AZAM

YANGA 1- 1 AZAM

E-mail Print PDF

VIEWED 1268 TIMES

Young Africans imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Azam FC katika mchezo wa wa Ligi Kuu Tanzania bara uliofanyika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kufikisha poniti 40 ikiwa ni poniti nne nyuma ya Azam yenye ponti 44 lakini wauza ramba ramba wakiwa mbele kwa mchezo mmoja.

Kikosi cha mholanzi Hans Van der Pluijm kimeshindwa kuzitumia vizuri nafasi za wazi katika mchezo na hasa kipindi cha kwanza baada ya mipira yao kuokolewa na mlinda mlango wa Azam FC Aishi Manula.

Didier Kavumbagu aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 14 ya mchezo baada ya kumalizia mpira uliokuwa umekolewa na golikipa wa Azam baada ya krosi ya Saimon Msuva kuokolewa na mabeki wa Azam FC kabla ya mpira huo tena kumkuta mfungaji na kuukwamisha mpira wavuni.

Young Africans iliendelea kukosa nafasi za wazi kupitia kwa Hamis Kizza ambaye leo hakuwa vizuri kwenye mchezo baada ya kukosa nafasi mbili za wazi za kufunga huku Msuva na Okwi pia wkaishindwa kuzitumia vizuri nafasi hizo pia.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 1 - 0 Azam FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote kusaka mabao ya mapema lakini umakini wa walinzi wa timu zote ulifanya mchezo kuendelea kuwa nguvu sawa na hasa eneo la katikati kutawaliwa na viungo wa Yanga Frank Domayo na Hassan Dilunga.

Dakika ya 71 ya mchezo Hamis Kizaa aliosa penati baada ya mlinzi Said Morad kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari lakini Kiiza alipiga mpira ambao ulikoloewa na mlinda mlango Aishi Manula na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Erasto Nyoni wa Azam FC alitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu dakika ya 72 ya mchezo baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi Hashim Abdallah.

Dakika ya 84 mchezaji wa Azam FC Kelvin Friday aliyeingia kuchukua nafasi ya Hamis Mcha aliipatia timu yake bao la kusawazisha baada ya uzembe uliotokea kwa walinzi wa Yanga kushindwa kumkaba Kipre Tchetche aliyetoa pasi kwa mfungaji wa bao hilo.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 1 - 1 Azam FC

Young Africans: 1.Juma Kaseja, 2. Juma Abdul, 3. Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub "Cannavaro", 5.Kelvin Yondani, 6. Frank Domayo, 7.Saimon Msuva, 8.Hassan Dilunga, 9.Didier Kavummbagu/Mrisho Ngasa, 10.Hamisi Kizza/Hussein Javu, 11.Emmanuel Okwi

Azam FC: 1. Aishi Manula, 2.Erasto Nyoni, 3. Gadiel Michael, 4. Said Morad, 5. David Mwantika, 6.Kipre Bolou, 7.Himid Mao, 8.Salum Abubakari, 9.John Bocco, 10.Kipre Tcheche, 11.Hamis Mcha/Kelvin Friday

Last Updated ( Wednesday, 19 March 2014 17:46 )  

Facebook Twitter YouTube
  • FACEBOOK

  • TWITTER