VIEWED 3359 TIMES
Msafara wa timu ya Young Africans leo mchana umepata fursa ya kumtembelea Balozi wa Tanzania nchini Comoro Bw Chabaka Kilumnaga kufuatia mwaliko wa timu pamoja na viongozi katika hafla ya chakula cha mchana nyumbani kwake eneo la Itsandra Moroni.
Katika hafla hiyo Balozi Chabaka alishukuru timu ya Young Africans kwa kufika nyumbani kwake na kujumuika katika chakula cha mchana pamoja na maofisa wa ubalozi waliopo nchini Comoro na watanzania wengine wanaoishi kwneye kiswa cha Ngazija.
Katika chakula cha mchana leo nyumbani kwa Balozi Chabaka pia waliweza kuhuduruia Balozi wa Comoro nchini Tanzania Dr Ahmed El Balidou na Waziri wa Elimu nchini Comoro ambao kwa pamoja waliukaribisha msafara wa Young Africans na kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Nawakaribisha sana hapa Comoro mjisikie kama mpo nyumbani Tanzania, pili nilifurahishwa na ushindi katika mchezo wa jana ambao niliuhudhuria na mkaweza kuibuka na ushindi hiyo ilikuwa inaendeleza sifa nzuri ya timu ya Young Africans pamoja na nchi ya Tanzania kwa ujumla alisema "Chabaka".
Aidha Balozi Chabaka alisema anaitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika mchezo wake unaofuata dhidi ya Al Ahly na kusema timu ina nafasi nzuri ya kufanya vizuri na kusonga mbele kwa kuwang'oa vigogo hao wa soka barani Afrika.
Mkuu wa msafara Bw Ramadhani Nassib aliushukuru ubalozi wa kuikabilisha timu ya Young Africans nyumbani kwake kwa ajili ya chakula cha mchana na kuwatakia maisha mema na yenye mafanikio chini Comoro ambapo ndio kwanza Ubalozi umeanza miezi mitatu iliyipita.
Mwenyekiti wa mashidano ya Kimataifa wa klabu ya Young Africans Seif Ahmed "Magari" akiongea kwa niaba ya kkabu ya Young Africans pia alimshukuru Balozi Chabaka kwa jana kuja uwanjani kuipa sapoti timu na leo kwa kuialika kwa ajili ya chakula cha mchana.
Mwisho wachezaji wa Young Africans, Viongozi wake, Benchi la Ufundi pamoja na Mabalozi na maofisa waliomba dua kwa pamoja kutakiana kila la kheri na maisha mema kwa waliopo Comoro na watakaorejea nchini Tanzania.
Young Africans itandoka kesho kurejea nchini Tanzania majira ya saa 6 na nusu mchana kwa shirika la Ndege la Precison Air na kutua Uwanja wa JK Nyerere majira ya saa 8 mchana .



