You are here: Home NEWS Local News Tutawanyamazisha - Simba

Tutawanyamazisha - Simba

E-mail Print PDF
Mabingwa wa soka kwa nchi za Afrikia Mashariki na Kati na mabingwa wa Tanzania Bara YANGA, Mwishoni mwa wiki hii wanatarajia kushuka katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wakati itakapo pepetana na mahasimu wao Simba,ambayo kwa sasa wanaongoza ligi kuu ya Vodacom baada ya kufikisha point 27 katika michezo 11 alizocheza huku Yanga ikiwa nafasi ya pili ikiwa imefikisha point 21 sambamba na timu ya Azam yenye point 21 lakini ni ya tatu baada ya kuzidiwa idadi ya magoli ya kufunga.
Pambano hilo la kukata na shoka litatoa ubishi juu ya nani zaidi ikiwa ni jadi kwa timu hizi kila zinapokutana ,tambo na majigambo kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa timu hizo hujinadi katika kila kona ya maeneo.
Simba ambayo imeweka nadhiri ya kucheza ligi bila ya kupoteza mchezo hata mmoja kwakutofungwa imeanza kuingiwa na wasiwasi wa mchezo huo baada ya kutoa malalamiko katika vyombo vya habari ikidai eti haina imani na mwamuzi wa pambano hilo Oden Mbaga kwa kuwa alionyesha udhaifu wa kuikandamiza timu yao katika pambano la mchezo wa Ngao ya hisani iliyochezwa mwezi Augosti Mwaka huu ikiwa ni kiashirio cha kuanza kwa ligi ya msimu huu.
Katika pambano hilo Simba waiiibuka mshindi baada ya kuifunga Yanga mabao mawili kwa bila,mabao hayo mawili kwa upande wa Simba yalipachikwa kimiani na Haruna Moshi Boban pamoja na mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Zambia aliyesajiliwa msimu huu Felex Sunzu.
Hata hivyo Yanga iliendelea kujipanga wakati ligi ilipoanza Yanga ilianza kwa kuchechemea hadi ilipoanza kushika kasi na kufikia nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu ya Vodacom.
Yanga ikiwa inafundishwa na kocha kutoka Uganda,Sam Timbe aliweza kuleta mafanikio makubwa kwa kipindi cha miezi sita kwa kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Tanzania Bara na ubingwa wa kombe la Kagame.
Hata hivyo hivi karibuni Uongozi wa Yanga ulifanya mabadiliko katika benchi la ufundi kwa kumwajiri kocha Mserbia Kostadin Papic ambaye hii itakuwa mara yake ya pili kufanya kazi Jangwani. .
Timu ya Yanga imeendelea kujifua huku wachezaji wote 28 waliosajiliwa msimu huu wakishiriki katika mazoezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika viwanja tofauti.
Kwa upande wa wachezaji kupitia nahodha wa timu hiyo Shedrack Nsajigwa” Fuso” amesema kikosi chao kipo katika morali ya ushindi hivyo wachezaji wameonyesha uwezo mkubwa kipindi hiki cha maandalizi wakiwa wamepania kumchapa mnyama katika pambano hilo.
Last Updated ( Monday, 31 October 2011 20:00 )  

  • FACEBOOK

  • TWITTER