Kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati na Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans Sports Club,
kesho itashuka dimbani katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuikaribisha timu ya Simba katika mchezo wa ligi Tanzania bara (VPL). Mchezo huo unatarajiwa kuwa mzuri kutokana na Young Africans kuhitaji ushindi ili kuweza kupunguza tofauti ya pointi baina yake na Simba, Simba inaongoza ligi ikiwa na point 27 ikifuatiwa na Young Africans yenye 21.
Kocha mkuu wa Young Africans Kostadian Papic amesema wachezaji wote ni wapo fit na ari ya mchezo, hakuna majeruhi hata mmoja.
Mashabaiki wapenzi na wanachama mnaombwa kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yenu



